
Kipindi cha ujauzito mama na mtoto wake wanaweza kuendelea kuwa na afya bora kwa mama kufanya au kufanyiwa yafuatayo: Kula chakula cha kutosha chenye virutubisho. Mchanganyiko wa chakula chenye virutubishi kitamfanya mwanamke awe na nguvu na afya; aweze kupata nguvu za kujifungua na kumhudumia mtoto. Kama mwanamke mjamzito hali chakula cha kutosha ni vyema ahimizwe na ndugu pamoja na wanafamilia wanaomzunguka. Kumbuka mwanamke analazimika kula chakula cha kumtosha yeye na mwanae. Hivyo anahitaji kula chakula zaidi kuliko watu wazima wengine na siyo kidogo kuliko wao.. Wanawake wajawazito, kama watu wengine, wanahitaji mchanganyiko wa protini, mbogamboga,matunda, na wanga.
Pia wanapaswa kula mara nyingi zaidi, wakipata vyakula vidogo vidogo kati ya milo ya kawaida siku nzima.. Vyakula mchanganyiko hulinda afya ya mama na mtoto. Ambapo vyakula hivo vina faida mbalimbali kwenye mwili wa mama mjamzito kama ifuatavyo:. Kuzuia upungufu wa chembe nyekundu za damu (anemia). Anemia (upungufu wa chembe nyekundu kwenye damu) hutokea sana wakati wa ujauzito. Husababisha kujisikia mchovu kila mara. Anemia ni hatari zaidi hasa kwa akinamama wajawazito kwa sababu damu hupotea wakati wa kujifungua. Hii inaweza kuzidisha upungufu huo na kusababisha mama kupoteza maisha.
Zuia anemia kwa kula vyakula vyenye protini na wingi wa madini chuma, na pia kutumia dawa ya kuongeza madini chuma mwilini. Malaria pia inaweza kusababisha anemia na hivyo hutakiwa kutibiwa mara moja. Vyakula vyenye wingi wa madini chuma ni pamoja na: molasi (sukari guru), maini, samaki, mayai, mboga za majani.. Kuongeza wingi wa Asidi ya foliki. Ukosefu wa asidi ya foliki (au vitamini ya foleti) kunaweza kusababisha hitilafu katika umbaaji wa mtoto na hata ulemavu. Chagua dawa za kuongeza madini chuma mwilini ambazo zinajumuisha asidi ya foliki, au dawa za kuongeza foliki. Kuhakikisha unapata Vitamini A ya kutosha. Matunda na mbogamboga yakiwemo karoti na nyanya, Mboga za majani na matunda ya rangi ya chungwa huwa na vitamini A, kirutubishi ambacho kinahitajika kwa ajili ya afya ya macho. Mwanamke mjamzito anahitaji mbogamboga za majani na matunda ya rangi ya chungwa zaidi kwa sababu vitamini A anayokula hutumika kwanza kukidhi mahitaji ya mtoto. Ukosefu wa vitamini A unaweza kusababisha kutoona usiku au upofu kwa ujumla.. Kupata mda mwingi wa Kupumzika. Mama mjamzito anatakiwa kupata mda mwingi wa kupumzika na kufanya mazoezi madogodogo kwa ajili ya kuweka mwili mwili wake kwenye hali nzuri.Kumbuka Kulea ujauzito ni kazi kwa mwili; nao mwili unahitaji kupumzika. Epuka Matumizi ya Bidhaa Hatari. Mama mjamzito anatakiwa kuepuka matumizi ya vitu hatarishi kama sigara, tumbaku, pombe na vinywaji vingine vyenye wingi wa caffein kama kahawa, hata soda.. Sigara na tumbaku huathiri mapafu ya mama na vinaweza kusabisha saratani na hata kifo. Moshi unaweza kusababisha mtoto kuzaliwa kabla ya muda wake au akiwa na uzito mdogo sana, au akiwa amekwisha kufa. Akina mama na watoto wao wanaweza hata kudhurika kutokana na watu wanovuta sigara karibu nao. Kwa hio ni vyema kuikumbusha familia na watu wengine kuepuka kuvuta sigara katika chumba kimoja au kweye gari wanapokuwa na mama mjamzito au watoto..
Pia vilevile Mama mjamzito anapokunywa pombe, pombe hiyo huenda kwa mwanae na inaweza kusababisha hitilafu za kudumu kwenye ubongo wa mtoto na mwili wake. Kadri anavyozidi kunywa pombe nyingi ndivyo madhara kwa mtoto yanavyongezeka.. Vivyo hivyo, madawa ya kulevya yakiwemo kokeni, bangi, unga na madawa mengine ni hatari kwa akinamama wajawazito na watoto wao.. Madawa ya kawaida. Dawa nyingi anapozitumia mwanamke mjamzito pia humfikia mtoto wake. Kwa sababu watoto tumboni wanakuwa wadogo sana na wakiendelea kuumbika, dawa ambazo ni salama kwa mtu mzima zinaweza kusababisha hitilafu wakati wa kujifungua na hata madhara kwa mtoto. Hivyo akina mama wajawazito wanapaswa kuepuka kutumia dawa kiholela bila kufuata ushauri wowote toka kwa daktari.Ambapo ni bora zaidi kuepuka madawa wakati wa ujauzito.. Epuka kukutana na wagonjwa. Kuugua wakati wa ujauzito ni tatizo kubwa kwa mama mjamzito. Ugonjwa unaweza kuleta shida katika kula, na pia kumfanya mtu kutokula chakula cha kutosha ambapo hili litapelekea kumnyima mwanamke mjamzito nguvu. Kwa hio ni vyema kuepuka kukutana na wagonjwa ili kupunguza uwezekano wa kuambukizwa.. Ugonjwa wa Rubella ambao ni aina ya surua kawaida siyo hatari sana kwa binadamu. Lakini unapompata mama mjamzito unaweza kusababisha hitilafu katika viungo na hata ulemavu kwa mtoto akiwa tumboni. Katika kumlinda mtoto, mwanamke mjamzito anapaswa kuepuka watu wenye upele, hasa watoto, ambao mara nyingi hupatwa maambukizi hayo. Hata watoto wengine wa mama mjamzito ambao wanaumwa wanapaswa kuhudumiwa na wanafamilia wengine au marafiki.. Mwanamke mjamzito anapaswa kuchanjwa dhidi ya pepopunda (tetanasi) mapema iwezekanavyo kati
ka katika kipindi ujauzito. Anatakiwa kupewa chanjo nyingine wiki 4 baadaye iwapo atakuwa hajapata chanjo zote. Hii husaidia kuwalinda wote wawili-mama na mtoto wake.. Pima magonjwa yote hatarishi kabla ya kuamua kushika mimba na kipindi cha ujauzito.. Vipimo vinaweza kugundua baadhi ya magonjwa mengi ambayo ni hatari kwa wanawake na watoto wachanga. Vipimo hivi humtahadharisha mama mjamzito kuanza matibabu mara moja, hatua ambayo inaweza kuzuia matatizo makubwa wakati wa ujauzito na baada ya kujifungua.. Ni busara kufanya vipimo dhidi ya: Anemia, kaswende, na malaria. Kumbuka kipimo cha VVU kinatakiwa kufanywa kwa akina mama wote wajawazito. Mwanamke anapogundua ana VVU, anaweza kuanza kutumia dawa ya kumsaidia afya yake na kumlinda mtoto asiambukizwe VVU..

0 Comments