TUZIFAHAMU KERO KWA MAMA MJAMZITO KIPINDI CHA UJAUZITO..


Ujauzito unaweza kusababisha matatizo mengi ambayo ni kero kwa mama mjamzito lakini siyo hatari. Mara nyigi inashauriwa kuepuka kutumia dawa kuondoa kero hizi.. Unaweza kuondoa kero hizi kwa urahisi kwa kutumia mbinu mbalimbali ukiwa nyumbani.




  1. . 1.Kichefuchefu. Hii ni kero mojawapo katika kipindi cha ujauzito ambapo mara nyingi husababishwa na tumbo lililo tupu. Kwa hio ili kuzuia kichefuchefu mama mjamzito anashauriwa kutokukaa na njaa kwa mda mrefu, Ambapo anatakiwa Kula vyakula vidogo vidogo, mara nyingi kwa siku. Ajaribu kula vyakula vyenye protini kama vile njugu, karanga, jibini, au nyama kabla ya kwenda kulala ili kubaki na chakula tumboni usiku wote. Kula kitu kikavu, kwa mfano wali au mkate asubuhi hata kabla ya kutoka kitandani.. Kumbuka, vyakula vyenye mafuta, viungo, na vyakula vyenye harufu kali huzidisha kichefuchefu kwa mama mjamzito. Chai yenye tangawizi, chai ya rangi na ndimo vinaweza kusaidia tatizo hili la kichefuchefu.
  2. . 2.Kiungulia. Kiungulia ni jambo la kawaida katika ujauzito. Ambapo maranyingi husababishwa na tindikali iliyopo tumboni, Ambapo ikipanda kifuani kwa mama mjamzito hufanikiwa kusababisha kiungulia.. Mabadiliko ya homoni na mtoto ambaye anazidi kukuwa husukuma tindikali iliyopo tumboni kwenda kifuani, na kusababisha kiungulia kwa mama na maumivu.
  3. . 3.Kupata choo kigumu na kwa shida, na bawasiri. Wanawake wajawazito mara nyingi hupata shida katika kujisaidia haja kubwa. Kufunga choo huwasabishia kero kubwa sana.. Kusukuma sana ili kutoa kinyesi kigumu huweza kusababisha tatizo lingine linalojulikana kama bawasiri. Bawasiri ni mishipa iliyovimba inayozunguka unyeo. Bawasiri husababisha muwasho, maumivu, au kuvuja damu yenye rangi nyekundu inayon’gaa.
  4. . 4.Uchovu. Mara nyingi wanawake husikia uchovu zaidi wanapokuwa na ujauzito kwa sababu miili yao inahitaji kupumzika zaidi. Hii ni hali ya kawaida kwa mama mjamzito. Ambapo anachotakiwa kufanya ni kupumzika zaidi na kusinzia kidogo kila anapoweza.. Hata hivyo, uchovu kupita kiasi unaweza kuwa dalili ya anemia, jambo ambalo hutokea sana, ila inakuwaga ni hatari kwa afya katika ujauzito. Kula vyakula vyenye kiwango kikubwa cha madini chuma kama vile nyama, maharagwe, mbogamboga, nafaka za jamii ya choroko, dengu nk. Pia tumia dawa ya kuongeza madini chuma mwilini ambapo zinapatikana kwenye maduka ya madawa.
  5. . 5.Kuvimba miguu na mikono. Hili ni tatizo lingine linalowakumba mama wajawazo ambapo wengi wamekuwa wakiogopa na kuona kama wanaugonjwa fulani. Ili kuepuka tatizo hili inashauriwa kupumzika na kuinua miguu yako juu kila siku, hasa iwapo utakuwa unatumia muda mwingi ukiwa umesimama au ukitembea. Epuka vyakula vilivyofungashwa au kufungwa kwenye makopo viwandani — mara nyingi huwa na chumvi nyingi, ambayo huzidisha uvimbe.. Kumbuka, unapoamka asubuhi au ukijikuta umevimba kila mahali, pamoja na usoni, huenda hizi ni dalili za hali inayotangulia kifafa cha mimba. Kwa hio inashauriwa kupima shinikizo la damu haraka iwezekanavyo, na hata kama ni salama, endelea na utaratibu wa kupima angalau mara moja kwa wiki kwa kipindi chote cha ujauzito.
  6. . 6.Hisia juu ya tendo la ndoa.. Hisia juu ya tendo la ndoa zinaweza kubadilika wakati wa ujauzito. Baadhi ya wanawake wajawazito hawapendi kufanya kitendo hiki, lakini wengine hutamaani kufanya zaidi kuliko kawaida. Hali zote hizi ni kawaida.. Kufanya tendo la ngono hakutamuathiri mwanamke au mtoto, lakini mwanamke mjamzito na mwenza wake wanaweza kujaribu namna tofauti zinazofaa za kufanya tendo la ngono bila kero.. Iwapo mwanamke, katika mimba zake zilizotangulia, alianza kupata uchungu wa uzazi mapema, ni vyema kuepuka kufanya ngono baada ya mwezi wa 6 kunaweza kusaidia asiingie kwenye uchungu wa uzazi mapema mno katika kipindi hiki. .

Post a Comment

0 Comments