
Wanawake wengi wanashindwa kutambua kama wana mimba au hawana, kutokana na kutokuwa na ufahamu wa mabadiliko yao yanayotokana na ujauzito.Dalili hizo ni kama:.
- 1.KUKOSEKANA KWA MZUNGUKO WA HEDHI. Wanawake wengi wanajulikana kama wanamimba kwa kutumia njia hii, ambapo hujikuta wakikosa hedhi zao.
- 2.KUTOKWA NA MAJI UKENI. Kutokwa na maji haya ni dalili mojawapo ya mimba ya mapema, kwani uke hutanuka baada ya mimba kutungwa. maji haya ni ya rangi ya maziwa..
- 3.MABADILIKO KATIKA MATITI. Kwa mwanamke mwenye mimba, matiti yake huongezeka ukubwa na kujihisi kama amebeba mzigo kifuani. Pia weusi hutokea kwenye chuchu zake za titi.
- 4.KUPATWA NA HEDHI NYEPESI. Haya ni majimaji ambayo kwa kiasi kikubwa yana rangi ya dhambarau na hutokwa kwa uchache sana ukiringanisha na yale maji ya hedhi ya kawaida ambayo ni mekundu kama damu. Utokwaji wa maji haya huambatana na maumivu madogo ya nyonga, na huchukuwa muda mfupi hata siku moja au masaa kadhaa..
- 5.MABADILIKO KWENYE USO Uso wa mtu mwenye mimba hutokwa na madoa meusi kutokana na mabadiliko ya hormoni kwenye mwili..
- 6.KUTAPIKA NA KUHISI KICHEFUCHEFU. Hii pia ni dalili ya kawaida iloyozoeleka miongoni mwa watu, kwani mwanamke hujihisi kutapika haswa wakati wa asubuhi kutokana na mabadiliko kwenye homoni ya oestrojeni. Dalili hii hutokea ndani ya wiki 2 hadi 8 baada ya mimba kutumgwa..
- 7.TAMAA YA KULA CHAKULA CHA AINA YOYOTE. Mtu mwenye mimba hujikuta na hamu ya kula chakula cha aina yoyote hata kama mwanzo alikuwa hakipendi.
- 8.KUONGEZEKA KWA TUMBO. Hii inatokana na kujaa kwa gesi tumboni ambapo mtu mwenye mimba hujihisi kama tumbo limeongezeka mara mbili..
- 9.UCHOVU. Mtu mweye mimba hupatwa na uchovu mara kwa mara kutokana na uzalishaji mkubwa wa homoni ya PROJESTERONI.
- 10.KUKOJOA MARA KWA MARA. Dalili hii pia hutokea kwa mwanamke mwenye mimba kubwa. Dalili hii hutokea ndani ya wiki 6 hadi 8 baada ya mimba kutungwa..
- 11.MAUMIVU YA MGONGO PAMOJA NA UGUMU WA KUPUMUA.
- 12.KUHISI KIZUNGUZUNGU. Mtu mwenye ujauzito pia huhisi kizunguzungu kutokana na mabadiliko ya homoni ambayo hupelekea kubadilika kwa msukumo wa damu mwilini ambapo huweza kupelekea mtu kuzimia..

0 Comments