
Mwanamke mjamzito anapokuwa na afya nzuri na kupatiwa matunzo yanayohitajika, kuna uwezekano kuwa ujauzito wake utakuwa wenye afya pamoja na mtoto akayezaliwa. Akina mama, wakunga na wafanyakazi wa afya wanaweza kufanikisha afya bora inayohitajika wakati wa ujauzito kwa kuzuia, kutibu, au kutoa msaada kwa ajili ya matatizo kama yatajitokeza.. Ujauzito unapofikia miezi 4½, mama anaweza kusikia mtoto akijigeuza, Ambapo daktari au mfanyakazi yeyote wa afya anaweza kusikiliza mapigo yake ya moyo kwa kutumia kifaa kiitwacho fetoskopu ambacho huwekwa juu ya tumbo la mama mjamzito.
. Je Mtoto atazaliwa lini?. Siku hii kitaalamu tunaiita DUE DATE (au siku ya matazamio), Ambapo mama mjamzito anakuwa anakadiria siku ambayo atakuja kujifungua. Kuitambua siku hii kuna njia mbili, ambapo njia zote zina tegemea mzunguko wa hedhi wa mama mjamzito.. Njia ya kwanza inahusisha kuongeza siku 280 (au wiki 40) kutoka siku ya kwanza ya mzunguko wako wa mwisho kwenda hedhi kabla ya kutokuziona siku zako.. Njia nyingine inahusisha kujumlisha miezi 9 na kuongeza siku 7 kwenye siku ya kwanza ya hedhi ya mwisho. Kwani Ujauzito huchukua takriban miezi 9 (miandamo ya miezi 10 au wiki 40). Hiyo ndiyo siku mtoto anatarajiwa kuzaliwa.. Kwa mfano, chukulia kwamba hedhi ya mwisho ya mwanamke ilianza Februari 30.. Februari 10 + miezi 9 = Novemba 10 Novemba 10 + siku 7 = Novemba 17 Tarehe ya mtoto kuzaliwa inatarajiwa kuwa Novemba 17.Watoto wengi huzaliwa kati ya wiki 3 kabla hadi wiki 2 baada ya tarehe hii..

0 Comments