DALILI HATARI WAKATI WA UJAUZITO

. Nenda kituo cha afya au hospitali kama utagundua moja wapo ya dalili za hatari kiafya zifuatazo.

Zinaweza kuhatarisha maisha ya mwanamke mjamzito.


  1. . Kuvuja damu kutoka ukeni:. Kuvuja damu kwa mama mjamzito kama inavyokuwa wakati wa hedhi, katika miezi ya kwanza ya ujauzito ni dalili ya kuipoteza mimba. Katika miezi ya baadaye katika ujauzito, uvujaji kidogo wa damu unaweza kuwa dalili kwamba kondo la nyuma linatengana na kizazi. Hii ni dharura, Kwa hio ni vizuri kutafuta msaada haraka iwezekanavyo.
  2. . Kupatwa na maumivu makali.. Maumivu makali katika miezi 3 ya kwanza ya ujauzito yanaweza kusababishwa na ujauzito kuota nje ya kizazi. Mama awahishwe hospitali mara moja. Maumivu makali katika miezi ya baadaye katika kipindi cha ujauzito au wakati wa kipindi cha uchungu wa uzazi yanaweza kuashiria kuwa kondo la nyuma linatengana na kizazi. Hii ni hatari, wahi hospitali haraka.
  3. . Kupatwa na homa kali. Homa kali (zaidi ya 39 sentigredi au 102 sentigredi) ni dalili ya maambukizi ambayo yanaweza kumuathiri mama au mtoto. Homa kali wakati wa ujauzito inaweza kusababishwa na mafua, malaria , maambukizi kwenye figo, maambukizi kwenye kizazi, au ugonjwa mwingine ambao husababisha homa.
  4. . Kupatwa na shinikizo la damu la juu (presha kupanda). Shinikizo la damu la juu (140/90 au zaidi), ikiambatana na maumivu makali ya kichwa, na uso kuvimba sana ni dalili za hali inayotangulia kifafa cha mimba. Shambulio ambalo linaweza kujumuisha mtikishiko wa maungo wa ghafla linaweza kusababishwa na kifafa cha mimba. Muwahishe mama hospitali au kituo cha afya mara moja..

Post a Comment

0 Comments