Faida ni kama zifuatazo:
1.HUSAIDIA UCHUNGU WA UZAZI ULIOKUWA MZURI NA KUPONA MAPEMA; kufika kileleni wakati wa tendo la ndoa huambatana na kubana kwa misuli ya nyonga hii husaidia kuweka imara misuli ya nyonga ambayo ni muhimu sana wakati wa kusukuma mtoto na baada ya kuzaa kwani misuli hii ikiwa legevu mwanamke huweza kushindwa kuzaa kwa njia ya kawaida na hata baada ya kuzaa huweza kushindwa kuzuia mkojo usitoke wenyewe au kuvuja damu kwa muda mrefu.
2.HUTIBU TATIZO LA KUFIKA KILELENI KWA SHIDA; kipindi cha ujauzito chuchu za mwanamke na kinembe chake huvimba na kuongezeka hisia mara dufu huku kiwango cha homoni za oestrogen kikiwa juu sana, hii humfanya kufika kileleni kirahisi sana kuliko mwanzoni.
3. HUMPA MAMA MJAMZITO UWEZO WA KUJIAMINI; kipindi cha ujauzito mwanamke hua anapata hofu sana na kutojiamini na mwili wake, hua na wasiwasi kwamba mwili wake unaharibika hivyo kitendo cha mwanaume wake kuendelea kushiriki naye tendo la ndoa humpa kujiamini kwamba mwili wake bado uko kwenye hali nzuri na anapendwa.
4.HUPUNGUZA MSONGO WA MAWAZO ; kipindi cha ujauzito wanawake wengi huwaza sana kuhusu kesho yao...je swala la uchumi litakuaje? mwili wangu utakuaje? je ntapata jinsia nayotegemea? na kadhalika.. tendo la ndoa hutoa homoni ya upendo kwa jina la oxytocin, homoni hii hupunguza mawazo na kumpa amani mjamzito.
5.HUPUNGUZA TATIZO LA KWENDA OVYO KUKOJOA AU KUJIKOJOLEA; wakati wa ujauzito mtoto anapozidi kua mkubwa anazidi kukandamiza kibovu cha mkojo, hii humfanya mama aende chooni kukojoa mara kwa mara na wakati mwingine hata akipiga chafya au kukohoa basi mkojo unaweza kutoka wenyewe. tendo la ndoa huibana misuli ya nyonga na kuzuia hali hii.
6.HUZUIA UWEZEKANO WA KUPATA KIFAFA CHA MIMBA; tafiti zinaonyesha kwamba aina ya protini inayopatikana kwenye mbegu za mwanaume huongeza kinga ya mwili na kuzuia uwezekano wa kupata kifafa cha mimba ambacho kinaua wanawake wengi sana.
7.HUMUANDAA MAMA MJAMZITO NA UCHUNGU; ukishiriki ndoa wakati wa tarehe zilizokadiriwa zimefika unapata homoni moja kutoka kwenye mbegu za mwanaume kwa jina la prostglandin, homoni hii huivisha mlango wa uzazi na kuanza kufunguka taratibu kujiandaa na uchungu.
8.HUTIBU TATIZO LA KUKOSA USINGIZi; wanawake wengi wajawazito hua na dalili mbalimbali za maumivu na kuumwa sehemu tofauti za mwili na msongo wa mawazo, hii huweza kuwakosesha usingizi kabisa..tendo la ndoa huweza kuwapa usingizi mzuri.
9.HUPUNGUZA PRESHA YA DAMU; kipindi cha tendo la ndoa presha ya damu hushuka kwenye kiwango kizuri sana, hii ni muhimu sana kwa wanawake wenye hatari ya kupata kifafa cha mimba kama wanene sana, wenye kisukari au wenye historia za ugonjwa wa presha kwenye koo zao.Kumbuka, kufika kileleni kwa mwanamke ni tiba kubwa sana haswa kwenye matatizo yanayohusisha tumbo.


0 Comments