JE NI VYEMA MAMA MJAMZITO KUFANYA TENDO LA NDOA

Kumekuwa na mkanganyiko mkubwa juu ya tendo la kufanya mapenzi, pindi mwanamke anapokuwa mjauzito. Ukweli ni kwamba hakuna tatizo lolote kwa mwanamke kuendelea kufurahia mapenzi na mumewe au mpenzi wake wakati anapokuwa mjamzito.

Wataalamu wanaeleza kuwa, ikiwa ujauzito ulioubeba haukupi shida yoyote ile na unajisikia uko poa, basi hakuna hatari yoyote ile ikiwa utataka kufanya.

Tatizo pekee ambalo huwa linawakumba wengi wa wanawake wakiwa wajawazito ni kuwa, huwa wanapoteza hamu ya tendo lenyewe wanapokuwa katika hali hii, au kushindwa kumudu kutokana na kujisikia uchovu muda mwingi. Ingawa pia wapo wanawake ambao wakiwa katika hali hii ndio kwanza, wanakuwa wanajisikia kukereketwa huko kwenye uke kupita maelezo, na wanatamani muda wote wafanye mapenzi.

Wapo baadhi ya wanawake ambao wanakuwa wako kawaida kimwili, lakini kisaikolojia wanakuwa na ile hofu ya kuwa kufanya kunaweza kuwaharibia mimba zao, fikra ambazo huwatoa kabisa katika mstari wa kufurahia tendo hili.Kiumbe kilicho tumboni wakati wa ujauzito huwa kinakingwa na ute maalum unaojulikana kitaalamu kwa jina la "amniotic fluid" ndani ya mji wa uzazi, pamoja na kuta za mji wenyewe wa uzazi.

Hakuna namna ambavyo uume unaweza kupita na kufika mahali mtoto anapokuwa anakua huko ndani, au zile mbegu kuwa zitapita moja kwa moja na kwenda kumdhuru mtoto.Kwa hiyo, ikiwa mwili wako uko poa, na madaktari wamekwambia kiumbe kinakua bila shaka, na unaweza kwenda kazini, huna haja ya kujibania utamu wa mumeo.

Post a Comment

0 Comments