Ugonjwa wa UTI una dalili nyingi na huenda nyingine zikafanana na dalili za malaria. Miongoni mwa dalili hizi ni;-
1.Maumivu wakati wa haja ndogo
2.Kutowa mkojo mchafu. Mkojo unawea kuwa na rangi sana, ua kama wa mawingu na kadhalika.
3.Harufu kali sana ya mkojo.
4.Mkojo kuwa na damu
5.Kukojoa marakwa mara hata kama mkojo utakuwa ni mchache sana.
6.Maumivu ya mgongo na tumbo kwa chini.(lower abdomen)
7.Maumivu ya kichwa.
8.Kuhisi uchovu sana
9.Miwasho sehemu za siri.
BAADA YA KUANGALIA DALILI, NJOO TUANGALIA JINSI YA KUJIKINGA NA UGONJWA HUU.
1.Jisafishe kutokea mbele kuelekea nyuma baada ya kukidhi haja kubwa (kwa wanawake). Hii husaidia kuzuia bakteria wanaotoka kwenye utumbo mkubwa wasipate nafasi ya kuingia kwenye njia ya haja ndogo.
2.mwaga maji kila uingiapo chooni kwaajili ya nkujisaidia. Kitendo hiki kitaondosha vijidudu vilivyopo pale chini.
3.Jisafishe sehemu za siri kabla ya kuingiliana na baada.
4.Hakikisha unakwenda kutoa haja ndogo (kukojoa) baada ya tendo la ndoa. Kitendo hiki kitasaidia kuondosha vijidudu vilivyoingia wakati wa tendo.
5.Nenda katoe haja ndogo haraka sana baada ya kuhisi.
6.Kunywa maji mengi zaidi. Husaidia kuondowa vijidudu kwa njia ya mkojo.
7.Vaa nguo za ndani za pamba, kavu na zisizobana.nguo za mpira na zinazobana husababisha jasho (majimaji) sehemu za siri. Majimaji haya husaidia bakteria kukuwa na kuishi hivyo wanaweza kuathiri njia ya mkojo.
Itambulike kuwa ugonjwa wa UTI unatibika bila ya matatizo. Jambo la msingi ni kuwa wagonjwa wengi wamekuwa hawamalizi dozi. Kwakuwa ugonjwa huu umeenea sana na ni rahisi kuupata imetokea hali za kujirudia rudia. Hivyo mgonjwa ni muhimu kuchukuwa tahadhari tulizo

taja hapo juu wakati akiwa anatumia dozi.
0 Comments